Monday, August 14, 2017

Serikali inavyoboresha huduma kupitia mifumo ya Tehama

Na Ofisi ya Habari,Kishapu

Serikali inatekeleza dhamira yake ya kuhakikisha inawapa wananchi huduma bora kwa wakati na ufanisi ili kuboresha maisha yao kielimu, kiafya na kiuchumi.

Hayo yanafanyika kwa ushurikiano mkubwa na wadau mbalimbali wa maendeleo kutoka ndani na nje ya nchi ili kufanikisha utoaji huo wa huduma hizo muhimu za kijamii.

Inatoa kipaumbele katika huduma za afya na elimu zenye ubora na zinazowafikia wananchi wote ili kuboresha maisha yao kwani afya na elimu bora kwa wananchi ndiyo raslimali muhimu kwa maendeleo.

Maendeleo ya Taifa letu la Tanzania yataletwa na wananchi wenye afya na elimu na wenye uwezo wa kuzalisha mali. Katika kuhakikisha hilo Serikali imeendelea kushirikiana na  wadau mbalimbali kutoa huduma za afya kwa kuzingatia sera na miongozo iliyopo.

Hivi karibuni Serikali ilizindua mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma au Public Sector Systems Strengthening (PS3) ukiwa na lengo kusaidia kufanikisha utoaji huduma bora hasa kwa wananchi walioko maeneo ya pembezoni.

Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kupitia ufadhili wa Shirika la Kimataifa la Watu wa Marekani (USAID) inatekeleza mradi huo ikishirikiana na wizara zinazosimamia sekta za afya, elimu na rasilimali fedha.
Utekelezaji wa mfumo huo unaolenga kupeleka fedha moja kwa moja kwenye vituo vya kutolea huduma za afya na elimu, unatarajiwa kuanza rasmi Julai 2017 katika vituo vyote vya kutolea huduma za afya na elimu ambavyo vipo mikoa 13 inayotekeleza mradi huo.
Katika utoaji huduma hizi mashuleni au vituo vya kutolea huduma za afya vikiwemo hospitali au zahanati suala la matumizi ya rasilimali fedha halikwepeki.

Hii ni kutokana na umuhimu wake kwani ni sehemu ambazo hufanyika manunuzi mbalimbali yakiwemo ya vitendea kazi vya kufundishia, kujifunzia, vya kutolea tiba na dawa.

Hivyo ni muhimu kuwepo na usimamizi wa mzuri ili kuhakikisha fedha hizo zinazotolewa na Serikali kuwahudumia wananchi zinatumika kwa usahihi kwa maana ya ‘value for money’.

Kupitia mfumo huo mpya wa uhasibu na utoaji taarifa au Facility Financial Accounting and Reporting System (FFARS) utasaidia utekelezaji wa utoaji wa rasilimali fedha moja kwa moja vituo vya kutolea huduma.

Hii ni katika kuimarisha uhitaji wa kuwepo kwa usimamizi wa fedha katika ngazi ya vituo vya kutolea huduma hizo za afya na elimu katika maeneo mbalimbali ya halmashauri.  

Mfumo wa FFARS utaweza kuwapatia watoa huduma mfumo rahisi ambao utawawezesha kutunza taarifa za fedha zinazotolewa na zilizopo katika vituo vyao.  

Hivyo ufuatiliaji matumizi ya fedha hizo utakuwa rahisi katika kufikia malengo ya utoaji huduma na kuhakikisha yanaendana na sheria za ununuzi na utoaji taarifa. 

Taarifa hizi zitasaidia Serikali kuimarisha mfumo wa usimamizi wa fedha za umma na kuongeza uwazi hivyo watoa huduma watawajibika kwa  na wajibu kwa jamii wanayoihudumia.

Mfumo utatumika katika vituo vyote vya kutolea huduma ya afya na shule, na uhuishaji huu wa mfumo utarahisishia na kuongeza ufanisi katika mifumo ya Serikali ya Tanzania na kuboresha usimamizi na matumizi ya rasilimali za umma.

Ili kuhakikisha watoa huduma hizo muhimu, wadau ambao ni watoa huduma za afya na elimu hivi karibuni walipatiwa mafunzo mahsusi ili kuwajengea uwezo katika uhasibu na utoaji taarifa (FFARS).
Kwa kuanzia, Serikali inatarajia kuanza kuutekeleza mfumo mfumo huo mikoa 13 katika halmashauri zake 93 ambapo Shinyanga ni miongoni mwa mikoa hiyo kupitia halmashauri zake zote sita.
Katika makala haya Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga iliyonufaika na mradi huo anazungumzia kwa kina kuhusu mfumo wa FFARS.

Anatanabaisha kuwa unasaidia upatikanaji wa taarifa sahihi katika hesabu za mapato na matumizi katika halmashauri zetu tofauti na ilivyokuwa zamani.

Magoiga anasema kuwa kuundwa kwa mfumo huu kutasaidia kuhakikisha fedha za ruzuku zinasimamiwa vizuri na taarifa za matumizi yake zinatolewa kwa usahihi.

Anaongeza kuwa utaratibu huu mpya utakuwa ni kichocheo cha uwazi na uwajibika wa watendaji wa Serikali ambao ndio watoji wa huduma katika sekta za afya na elimu kwa wananchi.

Hii ni kutokana na kuwa vituo hivyo vya kutolea huduma vinakuwa na mfumo maalumu wa kuandaa taarifa za mapato na matumizi tofauti na ilivyokuwa zamani.

Ni dhahiri kuwa Serikali ina nia ya dhati ya kutoa hudumia bora kwa wananchi wake kwa ufanisi na hilo ndilo lengo lake linalotarajiwa kupitia fedha hizo.

Mkurugenzi mtendaji huyo anasema ni kweli kumekuwa na changamoto ya upatikanaji wa taarifa sahihi za rasilimali fedha katika vituo vya huduma.

Anasema kuwa kutokana na changamoto hiyo halmashauri hushindwa kutoa taarifa sahihi za matumizi ya ruzuku zinazotolewa katika vituo hivyo na wakati mwingine kusababisha hamashauri husika kupata hati ya mashaka kutoka kwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

“Awali hakukuwa na mfumo sahihi wa kusaidia kulizuia hilo lakini kwa mfumo huu mpya sasa utasaidia kuhakikisha kunakuwa na muundo maalumu wa kuhifadhi taarifa za mapato na matumizi.

“Naamini hii itaongeza uwazi na uwajibikaji wa vituo hivi vya kutolea huduma na hivyo kupunguza changamoto mbalimbali ambazo zilikuwepo awali,” anasema. 

Mfumo huo kielektroniki ili kuendana na wakati na mabadiliko ya teknolojia ambapo unafanya kazi sambamba ujazaji vitabu ulioboreshwa.

Hii ni katika kuweza kukidhi changamoto mbalimbali za miundombinu ikiwemo umeme na kutokuwa na upatikanaji wa mtandao kwa baadhi ya vituo vya kutolea huduma katika halmashauri mbalimbali.

Aidha, mara baada ya kujaza katika vitabu, takwimu hizo zitaingizwa katika mfumo kwenye ngazi ya Halmashauri na vituo kupatiwa taarifa ya vituo vyao.

Ni dhahiri kuwa vituo hivyo vitatoa taarifa sahihi ya mapato na matumizi ambazo zitasaidia mwananchi kuhoji pale atakapoona kuwa huduma zinazotarajiwa kupatikana katika vituo hazitolewi kulingana na ruzuku iliyotolewa.

Mradi wa PS3 umefanikishwa na Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi pamoja na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

Sehemu ya majengo ya Hospitali ya Wilaya ya Kishapu




Tuesday, July 18, 2017

Moto wateketeza bweni Bunambiyu sekondari, DC aagiza uchunguzi kubaini chanzo ufanyike

Mkuu wa wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Nyabaganga Taraba ameagiza uchunguzi ufanyike mara moja kubaini chanzo cha moto ulioteketeza bweni la wasichana shule ya sekondari Bunambiyu.
Tukio hilo lilitokea leo Jumatatu saa 2 asubuhi wakati wanafunzi hao wakiwa madarasani na kusababisha uharibifu wa vifaa vikiwemo vitanda 12, magodoro 36 na mali zao zote.
Taraba pia amewataka wanafunzi katika shule hiyo iliyopo kata ya Bunambiyu kutoa ushirikiano wa kawaida uchunguzi ukiendelea kufanyika ili kubaini chanzo cha moto huo
Kwa mujibu wa mwalimu wa shule hiyo, Lameck Manumbu pamoja na jitihada za wanafunzi na wanakijiji wa Bunambiyu kuzima moto huo hawakufanikiwa kwani ulikuwa umeshika kasi na kuteketeza bweni hilo linalotumiwa na wanafunzi wa kike 26.
Taraba akiwa katika eneo la tukio akiambatana na Mkurugenzi mtendaji halmashauri ya wilaya hiyo, Stephen Magoiga, baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama na wataalamu wa sekta mbali mbalimbali walifanya tathimini ya awali na misaada kwa wanafunzi.
Mkuu wa Wilaya na timu yake waliungana na Uongozi wa Shule, Ungozi wa Kata na Kijiji na wananchi majirani na shule na walifanya kikao cha kazi kutafuta chanzo cha moto na kutafakari hatua za haraka za kuchukua.
Kwa kushirikiana na uongozi wa shule walianisha mahitaji ya haraka kuwasaidia waathirika na kuwapatia makazi ya muda huku hatua za kuwanunulia shuka zote pamoja na baadhi ya mahitaji zilifanyika.

Mkuu wa wilaya alihamasisha mchango wa papo ambapo zilipatikana jumla ya sh. 272,000 ambazo walipewa waathirika na kila mmoja alipata 10,000 kwa ajili ya mahitaji ya haraka wakati wakisubiri mahitaji mengine ya awaida ili waendelee na masomo wakati wakiwasiliana na wazazi wao.







TANGAZO LA KAZI

HALMASHAURI YA WILAYA YA KISHAPU
TANGAZO LA KAZI ZA MKATABA


Mkurugenzi mtendaji Wilaya ya Kishapu anawatangazia wananchi Raia wa Tanzania wenye sifa ya kuomba nafasi za kazi za mkataba kama ifuatavyo:-
1.     Msaidizi wa Hesabu ( Accounts Assistant ) – Nafasi 4
i.                   Sifa za Mwombaji
-         Elimu ya Kidato cha nne
-         Wenye cheti cha ATEC level II au “Foundation Level” kinachotolewa na NBAA.
ii.                 Majukumu/Kazi atakazokuwa anafanya
-         Kuandika na kutunza “Register” zinazohusu shughuli za uhasibu.
-         Kuandika hati za malipo na hati za mapokezi ya fedha.
-         Kutunza majalada ya Kumbukumbu ya hesabu.
-         Kupeleka nyaraka/barua za Uhasibu Bank.
-         kufanya usuluhisho wa masurufu, karadha, hesabu za banki na Amana.
iii.              Ngazi  ya Mshahara
-         mwombaji atayaebahatika kuajiriwa kwa mkataba ataanza na Mkataba wa malipo ya Tshs. 390,000 kwa mwezi ngazi ya TGS B
iv.              Masharti ya jumla ya muombaji kazi ya Mkataba.
-         Awe Raia wa Tanzania.
-         Awe na miaka 18-45.
-         Awe hajawahi kufukuzwa kazi, kupunguzwa, kuachishwa au kustaafishwa kazi katika Utumishi wa Umma.
-         Awe tayari kufanya kazi kituo chochote cha Afya ndani ya Wilaya ya Kishapu.
-         Mkataba utakuwa ni wa mwaka mmoja mmoja kwa kipindi chote cha mfadhili na Mkataba utarudiwa kulingana na utendaji kazi na maadili ya mtumishi.
-         Kipindi cha mfadhili kikikoma mtumishi hataingizwa moja kwa moja kwenye Ajira za Serikali.
-         Waombaji waambatishe vivuli vya vyeti vya Shule, Taaluma, Kuzaliwa na vitambulisho vya Taifa kwa wale walioandikishwa.
-         Kila mwombaji aambatishe na picha ndogo 2 passport size zilizopigwa hivi karibuni.
-         Siku ya usaili kila mwombaji afike na vyeti halisi vya shule, Taaluma, kuzaliwa na kitambulisho.
-         Kila mwombaji aandike kwa ushihi anwani yake na namba ya simu inayopatikana muda wote kwa ajili ya mawasiliano.
-         Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 27/07/2017
-         Maombi yote yaandikwe kwa mkono bila kuchapwa.
-         Maombi yote yawasilishwe kwa anwani ifuatayo:-
                       
                        Mkurugenzi Mtendaji (W)
                        S.L.P 1288
                        KISHAPU

NB:
Masharti yaliyoainishwa kwenye Tangazo hili yasomwe kwa makini na yazingatiwe



Stephen M. Magoiga
Mkurugenzi Mtendaji (W)
KISHAPU

Nakala:
1.     Katibu Tawala (M) – Kwa taarifa
2.     Mkuu wa Wilaya
3.     Waheshimiwa Madiwani – Watangazieni wananchi
4.     Watendaji Kata Wote – Tangazeni mbao za Matangazo
5.     Mbao za Matangazo zote Halmashauri ya Wilaya Kishapu.


Wednesday, July 12, 2017

Mbio za Mwenge wa Uhuru zilivyofana wilayani Kishapu



Na Ofisi ya Habari, Kishapu
Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 umepokelewa kimkoa kijiji cha Kinampanda kata ya Shagihilu katika wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga kutoka Simiyu na kuzindua miradi ya maendeleo yenye thamani ya sh. bilioni 3.7.
Katika mapokezi hayo Katibu Tawala Mkoa wa Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini alimkabidhi mwenzake wa Shinyanga, Albert Msovela ambaye alimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Kishapu.
Katika mbio hizo jumla ya miradi 12 ilizinduliwa ikiwemo ya kituo cha mafuta wenye thamani ya sh. milioni 337 kutoka kwa mjasiliamali Kija Ng’wani na mashine ya kusindika mafuta ya alizeti na unga wa mahindi sh. 244.
Mingine ni mashine ya kukoboa mpunga na kuweka katika madaraja sh. milioni 535.8 na ufugaji ng’ombe sh. milioni 400 ya mjasiliamli Mabela Masolwa pamoja na eneo la viwanda  lenye ekari 278 ambao thamani yake ni sh. bilioni 1.1.
Mradi wa ujenzi wa maji ya bomba kutoka Ziwa Victoria sh. milioni 755 uliofadhiliwa na shirika la Investing in Children and their Society (ICS), nyumba za walimu sh. milioni 55.8 uliofadhiliwa na mgodi wa Mwadui.
Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu iligharamia mradi wa pikipiki kwa vijana wajasiliamali wenye thamani y ash. Milioni 21, hudni zenye thamani y ash. Milioni 10.5 kwa wanawake wajasiliamali na utengenezaji bidhaa za ngozi wa Badimi sh. milioni 20.    
Akizungumza wakati wa mbio hizo, Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa, Amour Hamad Amour aliwataka Watanzania bila kujali tofauti zao kuuunga mkono jitihada za Rais John Magufuli katika kulinda rasilimali zilizopo nchini.
Alisema taifa litaongozwa kwa kufanya kazi kwa bidii ili tufikie malengo na maendeleo huku akiongeza kuwa tumezunguzkwa na mito na ardhi yenye rutuba ya hivyo wananchi wajitume.
Alipongeza wilaya kwa kuhakikisha inakuwa na viwanda huku akiwataka wananchi kutumia bidhaa zinazozalishwa wilayani badala yake kuwa tegemezi kwa bidhaa za kutoka nje ya nchi ili kukuza uchumi wa taifa.
Amour aliasa miradi inayozinduliwa na Mwenge iwaguse wananchi na waisimamie ili kuleta tija na ufanisi huku akipongeza pia kwa mapambano dhidi ya Ukimwi na rushwa.



















































SEARCH BLOG