Na
Ofisi ya Habari, Kishapu
Mwenge
wa Uhuru mwaka 2017 umepokelewa kimkoa kijiji cha Kinampanda kata ya Shagihilu
katika wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga kutoka Simiyu na kuzindua miradi ya
maendeleo yenye thamani ya sh. bilioni 3.7.
Katika mapokezi hayo Katibu Tawala Mkoa
wa Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini alimkabidhi mwenzake wa Shinyanga, Albert
Msovela ambaye alimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Kishapu.
Katika mbio hizo jumla ya miradi 12
ilizinduliwa ikiwemo ya kituo cha mafuta wenye thamani ya sh. milioni 337
kutoka kwa mjasiliamali Kija Ng’wani na mashine ya kusindika mafuta ya alizeti
na unga wa mahindi sh. 244.
Mingine ni mashine ya kukoboa mpunga na
kuweka katika madaraja sh. milioni 535.8 na ufugaji ng’ombe sh. milioni 400 ya
mjasiliamli Mabela Masolwa pamoja na eneo la viwanda lenye ekari 278
ambao thamani yake ni sh. bilioni 1.1.
Mradi wa ujenzi wa maji ya bomba kutoka
Ziwa Victoria sh. milioni 755 uliofadhiliwa na shirika la Investing in Children
and their Society (ICS), nyumba za walimu sh. milioni 55.8 uliofadhiliwa na
mgodi wa Mwadui.
Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
iligharamia mradi wa pikipiki kwa vijana wajasiliamali wenye thamani y ash.
Milioni 21, hudni zenye thamani y ash. Milioni 10.5 kwa wanawake wajasiliamali
na utengenezaji bidhaa za ngozi wa Badimi sh. milioni 20.
Akizungumza wakati wa mbio hizo,
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa, Amour Hamad Amour aliwataka
Watanzania bila kujali tofauti zao kuuunga mkono jitihada za Rais John Magufuli
katika kulinda rasilimali zilizopo nchini.
Alisema taifa litaongozwa kwa kufanya
kazi kwa bidii ili tufikie malengo na maendeleo huku akiongeza kuwa
tumezunguzkwa na mito na ardhi yenye rutuba ya hivyo wananchi wajitume.
Alipongeza wilaya kwa kuhakikisha
inakuwa na viwanda huku akiwataka wananchi kutumia bidhaa zinazozalishwa
wilayani badala yake kuwa tegemezi kwa bidhaa za kutoka nje ya nchi ili kukuza
uchumi wa taifa.
Amour aliasa miradi inayozinduliwa na
Mwenge iwaguse wananchi na waisimamie ili kuleta tija na ufanisi huku
akipongeza pia kwa mapambano dhidi ya Ukimwi na rushwa.